Aina Za Mbuzi Wa Maziwa

Aina ya mbuzi anayepatikana sehemu nyingi nchini ni Small East African Goat na hutoa kiwango kidogo sana cha maziwa. Hata hivyo mbuzi hawa wanaweza kuzalishwa na mbuzi wa kigeni ili kupata mbuzi wa aina ya hali ya juu wanaotoa maziwa mengi na wenye uwezo wa kustahimili magonjwa na hali ya anga ya hapa nchini.

Aina ya mbuzi wa kigeni wanaopatikana nchini ni kama vile:
  • Toggenburg, Boer, Saanen, British Alpine, German Alpine, Anglo Nubian,Angora na Oberhauzen.
  • Aina hizi zote za mbuzi hustahimili aina tofauti ya hali ya anga na huitaji mazingira tofauti ya ya kuwafuga.
Ikiwa unataka kufuga mbuzi wa maziwa ni bora kutafuta ushauri kutoka kwa wataalamu wa mifugo katika eneo lako ili wakufahamishe aina nzuri ya mbuzi wanaopatikana na mbinu nzuri za kuwazalisha zinazopatikana nchini.



























Jinsi Ya Kuwalisha Mbuzi Wa Maziwa

Ni muhimu kufahamu kuwa chakula unachomlisha mbuzi wako ndicho kitakachotengeneza maziwa hivyo basi ni muhimu:
  • Kumpa mbuzi chakula katika mahali palipo safi kwa sababu :
  • o     Mbuzi hula kila aina ya chakula hivyo usiwaruhusu kula chakula kilicho na mchanga 
  • o     Hali hii huwazuia kuambukizwa minyoo wanaopatikana kwenye mchanga
  • Mbuzi wa maziwa kwa mara nyingi hufugiwa kwenye zero grazing hivyo basi kumbuka kuwatengezea mahali pa kulia chakula na kunywea maji ambapo panahitajika kuwa juu na mbali na nyumba za kulala ili wasikanyage,au kuchafua chakula
  • Mbuzi mwenye uzani wa wastani huitaji takriban kilo 500 za chakula cha hali ya juu ama nyasi zilizokaushwa kwa mwaka huku kiwango cha kila siku kikiwa asilimia 5-7 ya uzani wake
  • Majani kama vile napier, majani ya mahindi au mtama, mboga zisizotumiwa na majani ya viazi yapaswa kukakatwa ili kupunguza uharibifu.
  • Ondoa chakula ambacho hakijatumiwa kutoka bandani mara mbili kwa siku.ikiwa mbuzi wako hubakisha chakula kingi hii ni ishara ya chakula duni,ama kupewa chakula kingi kupita kiasi,ama mbuzi wako hawana hamu ya kula chakula kwa sababu wana tatizo kama vile kutojihisi vyema
  • Wape maji safi ya kumywa kwa wingi kama lita 5 kwa kila mbuzi wa maziwa kwa siku
  • Waweza kuwapa mbuzi nafaka kama njia ya kubadilisha na chakula cha kawaida lakini kumbuka kubadilisha polepole wala si mara moja ili kuwaruhusu mbuzi kuzoea chakula kipya bila kuwadhuru.lakini tahadhari kuwapa mbuzi nafaka tupu kwani saweza kusababisha matatizo ya tumbo
  • Waweza kuwalisha mbuzi wa maziwa vyakula vya maziwa vinavyolishwa ng’ombe katika kiwango cha nusu kilo kwa mbuzi asiyekamwa,kilo moja kwa mbuzi wa kukama lita moja ya maziwa na nusu kilo kwa kila lita zaidi ya maziwa
  • Walishe mbuzi madini muhimu kulingana na kiwango cha maziwa wanachotoa















Share on Google Plus

About Suxiya Chinese language center

0 comments:

Post a Comment