Afya ya sungura wako


Ikiwa mfugaji atanufaika na sungura anaowafuga basi ni sharti ahakikishe wana afya nzuri. Kwani hii ndio changamoto moja kwa ufugaji wa sungura, magonjwa ya sungura hasa huwa ni ya tumbo na kifua. Na tatizo hasa ni kwamba wataalam bado hawaja gundua madawa ya maalum ya magonjwa ya sungura kwa hivyo ni muhimu kwa mfugaji kuhakikisha sungura wake hawapatwi na magonjwa. Sungura aliye na afya ni yule ambaye ngozi yake ninyororo, macho mazuri yasiyo na kasoro, asiye na vidonda vya ngozi, katika macho, midomo, au kwenye masikio. Uchafu kwenye miguu na mapua ni ishara ya ugonjwa wa kukohoa kwani sungura huosha mapua yake kwa kutumia miguu ya mbele. Pia unaweza kumuweka chini nakutizama dalili za ugonjwa anaporuka.

Biashara nzuri

Kulingana na Bw. Wachira ufugaji wa sungura una manofaa kwani yeye hufuga sungura kama biashara na sasa wakulima wengi humtembelea ili awafunze kuhusu ufugaji wa sungura. Huwauzia wale wanaotaka nyama ya sungura na pia wafugaji wanaotaka kufuga sungura. Bw. Wachira huuza sungura mmoja aliyechinjwa kwa shilingi kati ya 300 hadi 1,000 kulingana na uzito wake. Ingawa soko la nyama ya sungura haliko kwa wingi Bw. Wachira ana matumaini, ameweza kujiunga na wafugaji wengine na wamefungua hoteli mjini Murang’a ambapo nyama ya sungura huuzwa na pia huweza kuwauzia wafugaji wengine sungura wao mjini Nairobi. Pia ana matumaini kwamba huenda wakapata soko katika nchi ya uchina hivi karibuni.

Faida za kufuga sungura

Kulingana na wataalam, sungura ni mnyama rahisi wa kufuga hana gharama kubwa na ndiposa ni shughuli ambayo mkulima mdogo anaweza kuzingatia. Sungura akitunzwa vyema inavyostahili haugui kwa urahisi na pia lishe yake ni rahisi kupatikana. Chakula cha sungura ni kama nyasi, mamboga kama vile sukuma, spinarch, karoti, na pia unaweza kununua chakula halisi cha sungura kutoka maduka ya vifaa vya wanyama. Ingawaje kulingana na ujuzi wa Bw. Wachira anashauri mfugaji akaushe chakula cha sungura ili asikojoe ovyo na pia kukinga magojwa ya tumbo.
Nyama ya sungura ni tamu na wale ambao wameila huilinganisha na nyama ya kuku. Kulinagana na wataalam ni nyama nyeupe ambayo haina mafuta ya cholestrol na hiyvo wataalam wa lishe bora huhimiza matumizi ya nyama ya sungura kwani ni bora kwa afya.
Ufugaji wa sungura ni kitengo kidogo cha ustawi wa mifugo kwa minajili ya kuongeza uzalishaji wa nyama ya sungura, na pia kwa mapato. Kama mnyama yeyote sungura anahitaji utunzaji mwema ili waweze kuzalisha kwa wingi. Anahitaji kujengewa chumba maalum na kuangaliwa kila siku na kuhakikisha usafi wa vyumba hivi. Na kama watoto wa binadamu pia sungura wanahitaji kupewa chakula kisafi cha hali ya juu kilicho na madini ya protini na kalsham na pia kupewa maji masafi.

Pale utapata maarifa ya kufuga sungura

Bw. Wachira aliwatembelea maafisa wa mifugo katika wizara ya ustawi wa mifugo na kupata maelezo zaidi, pia aliweza kuhudhuria mafuzo kadhaa iliyoandaliwa na mashirika kadhaa ikiwemo Kenya Entrepreneur Development na wizara ya kilimo. Kwa wakati huu Bw. Wachira anafuga sungura kama biashara, ana idadi sungura kadri 500 na huuza nyama ya sungura kwa majirani na pia kwa mahabara ya vyuo vikuu ambayo kwa kazi ya utafiti. Matumaini yake ni kuweza kuuza nyama ya sungura kwa mahoteli makubwa na hata kupata soko la nchi za nje.

Uzalishanaji

Sungura wa kike aliyeshika mimba hujulikana kwa mwenendo wake, huwa mtulivu, na hula chakula kidogo. Baada ya siku 30 hadi 32 hujitoa manyoa yake kujenga kiota na huzaa siku chache baadaye. Sungura kwa mara moja huweza kuzaa kati ya mtoto mmoja hadi watoto 15. kulingana na Bw. Francis Wachira sungura anayezaa watoto wengi ni sharti awe na afya njema la sivyo watoto hawa wanaweza kufa kwa kukosa chakula chakutosha.



Share on Google Plus

About Suxiya Chinese language center

0 comments:

Post a Comment