Mzinga wa Langstroth ni mfano wa mzinga wenye fremu inayosonga na ndio hutumiwa kwa sana.Fremu zimetenganishwa kutoka kwa ukuta wa mzinga,na kwa fremu zingine na nafasi ya nyuki.Mizinga mingi ya Langstroth ina masanduku ya kuweka fremu kumi,lakini mizinga ya fremu nane –na kumi na mbili pia hutumiwa.Kama kigezo ukubwa na baadhi ya michoro hutofautiana kutoka kwa nchi hadi nchi ,ni muhimu kununua mizinga na vifuniko vya mizinga kutoka kwa muuzaji mmoja.
• Kifuniko cha juu ama paa
• Kifuniko cha ndani
• Chumba cha asali
• Chumba cha uzazi
• Ubao wa chini
• Ubao wa kushukia na stendi
Mzinga wenye ubao wa juu
Mizinga hii hutengenezwa kupunguza gharama na kama mbadala kwa mitambo na mizinga ya Langstroth.Ni maarufu kwa saababu ya urahisi wake na bei yake isiyo ghali,katika nchi zinazoendelea.Miziwnga yenye kibao cha juu pia ina fremu zinazosonga na hutumia wazo la nafasi ya nyuki.
Mzinga mwenye kibao cha juu unaitwa hivyo kwa sababu fremu za mzinga huu zina tuu kibao cha juu,na sio kibao cha kando ama cha chini.Mfugaji wa nyuki hatoi msingi(hutoa tu msingi mdogo)kwa nyuki kuanzia ujenzi.Nyuki hujenga sega kwa hivyo huning’inia chini kutoka ubao wa juu .
Tofauti na mzinga wa Langstroth,asali inaweza kutolewa kwa mwendo unaoenda nje kwa sababu fremu ya mziniga mwenye kibao cha juu hauhitaji msingi madhubuti ama fremu kamili.Kwa sababu nyuki hawana budi kujenga sega baada ya kila vuno,mzinga mwenye kibao cha juu huzalisha nta nyingi na asali chache.Hata hivyo kama mzinga wa Langstsroth,nyuki wanaweza kufanywa wahifadhi asali kando na sehemu wanayolea nyuki wachanga ili nyuki wachache wauawe wakati wa kuvuna asali kutoka kwa mzinga wenye kibao cha juu.
0 comments:
Post a Comment