nyuki

Nyuki ni wadudu wa familia Apidae wenye mabawa manne angavu na mwiba kwenye nyuma ya mwili wao. Hukusanya mbelewele na mbochi ya maua kama chakula chao. Spishi inayojulikana hasa ni nyuki-asali (Apis mellifera) ambaye hufugwa kila mahali duniani. Kuna spishi zaidi ya 20,000 zinazojumlishwa na biolojia kati ya nyuki lakini ni wale wa jenasi Apis wanaotengeneza asali inayovunwa kwa matumizi ya binadamu.

Umbo la nyuki

Mwili una pande tatu jinsi ilvyo kwa wadudu wote: kichwa mbele, kidari katikati na tumbo nyuma, halafu jozi tatu za miguu na jozi mbili za mabawa.
Mwili huwa na nywele na ina rangi kali za njano-nyeusi kama onyo kwa maadui.
Nyuma ya tumbo wanabeba mwiba wanaotumia kudunga wakijisikia wameshambuliwa. Wakidunga mwiba wanaingiza pia kiasi kidogo cha sumu katika kidonda. Sumu hii inasababisha maumivu na watu wengine wanaathiriwa vikali lakini si kila mtu. Kuna nyuki wanaokufa baada ya kudunga kwa sababu mwiba unabaki kwenye kidonda lakini wengine wanaweza kutoa mwiba na kudunga tena.
Share on Google Plus

About Suxiya Chinese language center

0 comments:

Post a Comment